bREAKING nEws: Method Mwanjale Sasa kumsaidia Kocha OMOG kuleta makombe Simba.. #share.

Mabingwa mara nyingi zaidi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,  Ligi ya Muungano na Kimataifa,.. Simba Sports Club ya Jijini Dar es Salaam, leo wametangaza mabadiliko makubwa katika kikosi chake kinachotarajia kuanza kuingia uwanjani kusaka upya ubingwa wa Ligi Na Makombe ya Kimataifa.



Katika 'press' iliyosambazwa mchana huu kwa Waandishi wa Habari, Benchi la ufundi la klabu ya Simba, chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.
Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu, beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba, akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho, ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu, Mohammed Hussein (Tshabalala) na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.

Klabu inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake mwandamizi, Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa Timu.

Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika kusini.
Ilimaliza Taarifa hiyo iliyosainiwa na Msemaji Mkuu wa Klabu hiyo Bw. Haji Sunday Manara.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search