mALIMWENGU: Zimamoto wamnasua nyoka aliemng'ata na kumjeruhi vibaya 'bosi wake' Nchini Marekani.. #share

JESHI la Zimamoto na Uokoaji mjini hapa, limelazimika kumuua nyoka mmoja aina ya boa ambaye alijiviringisha kwenye shingo ya mwanamke mmoja na kuanza kumng’ata usoni.


Kwa mujibu wa jeshi hilo, walilazimika kutumia kisu kukata kichwa cha nyoka huyo ambaye alikuwa akimng’ata mwanamke ambaye anadaiwa kumuokoa siku moja kabla ya tukio.

Mwanamke huyo alipiga simu ya mwito wa haraka na dharura kwa kikosi cha uokoaji, ambapo alisema; “Nisaidieni tafadhali. Kuna nyoka amenasa shingoni mwangu.”

Mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alikuwa na nyoka zaidi ya 11 aliwaokoa nyoka hao kutoka eneo lisilojulikana Jumatano wiki hii na kuwaleta nyumbani kwake.

Jeshi hilo lililazimika kumkimbiza mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 45 hospitalini, ili akapatiwe matibabu ya haraka na kisha kumtupa nyoka huyo kwenye debe la taka lililopo karibu na Sheffield Lake City Hall.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search