TETESI za Kispoti : Valverde 'agonga nyundo' uhamisho wa Neymar.. #share

Kocha mpya wa Barcelona Ernesto Valverde, ametupilia mbali uvumi mitandaoni unaomuhusisha mshambuliaji wake nyota Neymar kuhamia klabu ya Paris Saint-Germain.



"Naymar is with us and we absolutely want him to stay with us here..." alitonya Valverde..


..akiongeza,.. "yasemwayo mbali na haya nikwambiayo mimi chukulia kuwa ni uvumi tuu na uzushi usiokuwa na mbele wala nyuma.."  kocha huyo matata na mchezaji nyota wa zamani wa Barcelona, aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuelezea mikakati yake ya kuivaa Juvetus leo kwenye michuano ya ICC Champions Cup inayoendelea...

Neymar ni kipenzi cha mashabibiki awapo uwanjani, lakini nasi viongozi tunampenda sana.. na wachezaji wenzie wanampenda kwa busara zake, na ushawishi wake kwenye chumba cha kubadilishia mavazi.. alimaliza Valverde.. huku akimuangalia Neymar ambae punde tu akajiunga na vinara wenzake Mesi na Suarez kuendelea kupasha kwa ajili ya mechi yao na mahasimu wao Juventus 'vibibi kizee wa Turino..'

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search