News Updates:: Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amefikishwa Mahakamani mchana huu.. #share
New Updates:: Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.. Tundu Lisu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana huu kujibu mashtaka yake ambayo bado hayajawekwa wazi.
Wakati Lissu akifikishwa Mahakamani, kuna taarifa za makada sita wa CHADEMA ambao amekamatwa eneo la Kituo cha kati cha Polisi wakati wakifuatilia yanayojiri tokea kukamatwa kwa Rais huyo wa TLS ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki,
Hapo awali, afisa Habari wa Chadema Tumaini Makene, alibainisha uwepo wa uwezekano wa Lissu kupanda kizimbani kufuatia mazingira tofauti yanayohusiana na kukamatwa kwake..
Endelea kufuatana nasi kupitia www.matukio360.com kupata yanayojiri kadri ya tutakavyoyapokea...
No comments:
Post a Comment