FURSA: NEEC wametuletea 'weka akiba, nunua hisa' kuinua fursa kwa vijana... #share

VIJANA wametakiwa kuweka akiba na kununua hisa ili kuwekeza kwenye ujasiliamari kama njia ya kukabiliana na hali ya uchumu katika kipindi hiki ambacho kimekuwa na changamoto ya upatikaji wa ajira nchini.



Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Tanzania (NEEC), Beng’i Issa baada ya ufunguzi wa shindano la kuweka akiba na ununuaji wa hisa (DSE Investment Challenge) lililoandaliwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam na kushirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari.

“Kwa hivi sasa tunapoelekea uchumi unazidi kukua, hivyo vijana ndiyo wanategemewa kushiriki katika masuala ya uchumi na vijana wanapopata elimu hiyo ya kuweka akiba na kununua hisa ni vizuri,” alisema.

Aidha amesema kushiriki katika shindano hilo ni muhimu kwa vijana wa kitanzania kwani linawasaidia kupata elimu na kukuhamasisha ili kufahamu suala la uwekezaji wa kuweka akiba na kununua hisa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE Moremi Marwa alisema katika kipindi cha miaka minne tangu kuanzishwa kwa shindano hilo washiriki wamekuwa wakiongezeaka mwaka huu zaidi ya washiriki 12,300 ukilingana 4,000 walioshiriki mwaka jana.

“Tuanaona kwamba ushiriki unazidi kuongezeka, lakini vile vile katika shindano hili ni suala la kuongeza uelewa kwa wanafunzi na tumeona kwamba siku zinavyo kwenda hata uelewa katika suala la uwekezaji unazidi kuongezeka,” alisema.

Aidha amesema lengo la shindano hilo ni kuleta elimu pamoja na uelewa kwa wananchi kuhusiana na uwekezaji kwa kutumia wanafunzi ambao wataenda kushirikisha wazazi wao pamoja na walezi lakini na wao pia kwa kiasi kidogo walichonacho wanaweza kuwekeza.

Katika shindano hilo kwa upande wawashiriki wanafaunzi wa vyuo vikuu mshindi wa kwanza alikuwa ni Benson Macharo mhitimu kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo ambaye alipata zawadi ya sh. milioni 2.

Akizungumza baada ya ushindi huo amesema kwamba hii ni mara yake ya pili kushirika ambapo mwaka jana alishika nafasi ya tatu lakini hakukata tamaa akishiriki kwa mara ya pili na kuibuka mshindi wa kwanza.

Aidha mshindi kwa upande wa washiriki wanafunzi wa sekondari ni Irene David mhitimu kutoka shule ya sekondari Scolastica ya mjini moshi ambaye amejinyakulia zawadi ya sh. milioni 1.






About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search