Shocking News! Coplo Brayson afunguka mazito kesi ya SCORPION #share.. adai macho ya Saidi yalinyofolewa kwa vidole;

KESI dhidi ya Mshtakiwa Salum Njwete (Scorpion), ya kumjeruhu kwa kumtoboa macho Saidi Mrisho leo imeendelea kusikilizwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, ikiwa ni zamu ya shahidi wa nane Coplo Brayson aliefika Mahakamana hapo kutoa ushahidi akiwa kama mpelelezi wa kesi hiyo na ndie aliemchukua maelezo mshtakiwa na kusema alikili kuwa alimtoa macho kwa kutumia vidole vyake.


Mashtaka hayo yanaongozwa na wakili wa Serikali Nasoro Katuga mbele ya Hakimu Flora Haule ambapo Wakili huyo kwa upande wa jamhuri alianza maswali kwa Askari.


Shahidi huyo alieleza mahakamani hapo kuwa bada ya kupata taarifa za kujeruhiwa kwa mtu huyo ndipo walipochukua jukumu la kufanya upelelezi baada ya kutoka kuongea na mgojwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Alieleza kuwa baada ya kupata taarifa walienda baa ya Kimboka na kumuomba meneja wa Baa hiyo na mwenyekiti wa Ulinzi shirikishi na kuwauliza kama wanamfahamu mtu huyo ambapo walijibu wanamfahamu.

Shahidi alisema ndipo walipowaomba ushirikiano wa kumleta mtuhumiwa kituo cha Polisi Buguruni na waliweza kufanikisha zoezi hilo ambapo walimleta na walimkabidhi kwake na yeye kumpeleka kwa mkuu wa upepelezi.

Alieleza Mahakamani hapo baada ya hapo alikabidhiwa mshtakiwa na wakaingia chumba cha mahojianao tayari kwa kuanza kumhoji ambapo mtuhumiwa alikuwa akitoa maelezo na yeye alikuwa akimuhoji.

Shahidi alisema mshtakiwa alikiri kumjeruhi kwa kutumia kisu na kisha kumtoa macho yake kwa kutumia vidole kwakua mlalamikaji alikuwa akituhumiwa kwa kusumbua wananchi kwa wizi maeneo ya Buguruni.

Baada ya hapo Shahidi baada ya kumaliza maelezo hayo aliweka saini yake na kumtaka mshtakiwa athibitishe kwa kuweka saini yake ambapo alifanya hivyo.


Baada ya ushahidi huo Wakili wa utetezi wa upande wa mlalamikaji Nasoro Juma alikataa karatasi hiyo ya maelezo ya mteja wake isipokelewe mbele ya mahakama kwa kudai mshtakiwa alitoa maelezo hayo akiwa anafanyiwa mateso makali na kumfanya akubali.

Upande wa Jamhuri walipokea hoja hiyo na kusema watatoa majibu shauri hilo litakaporudi tena mahakamani hapo siku ya Agusti 2 mwaka huu.


By: Jemah Makamba.. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search