NEWS: Mufti ataka Waislamu wampuuze anaejifananisha na Mtume Eliasi .. #share..

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania limetoa limewataka Waislamu wote kutokumuamini Hamza Issa amabaye muumini wa dini hiyo kwa kujifananisha na Mtume Eliasi.


Baraza hilo limetoa wito kwa Masheikh wa Mikoa na Wilaya Nchini pamoja na Taasisi mbalimbali za kiislamu kutompa fursa mtu huyu katika jamii kwa kuongea au kuweka mihadhara ya kidini kwa lengo la kuhutubia jamii na kuipotosha.

Akizungumza Dar es Salaam leo,Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa (BAKWATA), Khamis Mataka kwa niaba ya Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi,alisema katika dini ya kiislamu hakuna Mtume wa mwisho zaidi ya Mtume Muhammad (S.A.W.)
Alisema Hamza ni muumini wa kislamu lakini anautumia umini huo katika kuwaaminisha waislamu kuwa yeye ni Nabii hali ambayo katika misingi ya dini ya kiislamu kile anachodai hakimo katika mafundisho ya Uislamu.

“Hivyo kudai kuwa yeye ni Mtume na kutumia maandiko ya uislamu katika upotoshaji mkubwa kabisa ambao ukiachwa bila kudhibitiwa ni kuruhusu fujo na uvunjifu wa amani,”alisema Mataka.
Baraza la Ulamaa lenye usimamizi mzuri wa maadili ya kiislamu linatoa wito kwa waumini wote kiislamu Mkoa wa Pwani hasa wa Misungusungu,kuendelea kuwa watulivu na kuaachia vyombo vya Usalama kufanya kazi yake ya kudhibiti na Kumshughulikia mpotoshaji huyo.

Pia Baraza hilo limewataka waislamu kufata mafundisho ya wazi katika dini hiyo kwa kutambua kuwa kila muislamu wa kada yeyote hakuna Mtume tena katika uislamu baada ya Mtume Muhammad (S.A.W).

“Baraza hilo linawataka waislamu kutomfata mpotoshaji huyo kwa kigezo cha kutumia dini hii kwa kujifananisha na Nabii aliyefariki na kusema roho yake imerudi kwake na kumuingia katika mwili wake,”alisema Mataka.

Aidha Mufti huyo ametoa wito kwa mtu huyo kuacha mara moja kutumia dini hiyo katika kujinadi kwa kushukiwa na roho ya Nabii huyo hali ambayo yeye si Mtume.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search