FURSA: Waziri Mahiga aja na boda To boda' 'kuwashika' Vijana.. #share

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Augustine Mahiga amewataka vijana kuchangamkia fursa za kibiashara ili kuweza kukuza uchumi na ukuaji wa viwanda vidogo vidogo katika kushirikiana na kuwa na umoja katika Nchi za Afrika Mashariki.


Akizungumza hayo Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kampeni ya Chungulia Fursa Boda to Boda,alisema Waziri kampeni hizo zina zina nia ya dhati katika kuwapatia vijana fursa katika kuwamasisha kuhusiana na biashara.

Alisema katika kila kanda Duniani wameona umuhimu wa kuungana katika kufanyabiashara hasa katika nchi zilizoendelea.

"Biashara ndio chimbuko la utajiri kwahiyo ili utengeneze fursa ya biashara lazima uwe na mtaji na mtaji ili ukuwe ni vema kuwa na viwanda,"alisema Mahiga.

Pia amewataka vijana na wakina mama kuchangamkia fursa za biashara katika kuwa na ushirikiano na umoja ili kuweza kukuza viwanda vyetu vya ndani na mahusiano ya kibiashara na Mataifa mengine.

Alisema hivyo Serikali yetu imeweza  kutatua migogoro na vikwanzo vya forodha visiweze kutofautiana na hadi sasa vikwanzo hivyo tumeshavivuka hivyo serikali ipo katika mpango wa kuandaa soko la pamoja kwa lengo la kukuza ushirikiano wa biashara za mipakani za jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Serikali ipo katika mpango mzuri wa kukuza biashara na kuunganisha soko la biashara ili kukuza uchumi na viwanda katika kunyanyua fursa kwa vijana na wakinamama hivyo tuko katika kuongeza ushirikiano na umoja na kutaka kuonganisha mfumo wa pamoja wa  vyuo vya Tanzania na Nchi za Masharikia kuwa na ada moja ili.kuwawezesha wanafunzi kusoma popote,"alisema Mahiga.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS,Francis Kiwanga alisema lengo letu ni kuwahamasisha vijana na wanawake kuzichangamkia fursa za kibiashara katika kukuza maendeleo ya Taifa,hivyo kampeni hizo zitafanyika katika mikoa mengine kwa ajili ya kuwa elimu na uhamasishaji wa kujiungana kujimuika katika umoja wa biashara za mipakani katika jumuiya hiyo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search