TOP NEWS: Mwigulu alivyowapa makavu live 'Wizara ya Maji..' ashangaa Zimamoto kutozwa bili ya maji.. #share.. Mahakama yapigilia 'msumari wa mwisho, yasema Habinder atibiwe Muhimbili.. TRA Yacharuka Mwanza.. Yafungia Vituo kibao vya mafuta.. na Evrton yatuma salamu za Upendo kwa Tanzania..

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  kuimarisha na kukabiliana na changamoto zilizomo ndani ya Taasisi hiyo muhimu kwa kutumia vyema rasilimali zinazopatikana ndani ya Taasisi hiyo.



Waziri Nchemba wakati akihutubia mkutano wa ndani wa Jeshi hilo chenye lengo la kurekebisha dosari zilizojitokeza na kujiwekea malengo ya kuboresha utendaji kazi kwa ujumla katika mwaka ujao wa kiutendaji. .

Moja ya vitu alivyogusia katika hotuba yake ya ufunguzi ni kututatua changamoto zinazowakabili jeshi la zimamoto likiwepo la baadhi ya vikosi vya jeshi hilo kuwachini ya wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukuzi (Bandari na Viwanja vya ndege) huku sheria mpya jeshi hilo ikitaka vikosi hivyo kuwa sehemu moja chini kamishna jenerali wa jeshi hilo

Kuhusu zimamoto kukatiwa huduma ya maji, Waziri Mwigulu amesema kuwa atakaa na Waziri mwenzake wa Maji kutatua tatizo hilo kwani kwa mujibu wa taratibu huduma hiyo inatakiwa kutolewa bure kwa vikosi vyake.. na akashangazwa na malalamiko ya kukatiwa Maji.. 


Kwa upande wake kamishna Jenerali wa jeshi la zimamoto akiongea kwenye Mkutano huo alimuomba Waziri Mwigulu kusaidia kutatua kero hizo za Maji na upungufu wa magari ili waweze kuendana na kasi ya Tanzania ya viwanda.


Mkutano huo wa siku mbili unafanyika Makao makuu ya Nchi Dodoma katika ukumbi wa LAPF



================ =============
Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili wafanyabiashara James Rugemalira na Seth Habinder wa IPTL imeahirishwa hadi tarehe 22 mwezi huu. 


Watuhumiwa hao walifikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo wakili wa serikali alisema upelelezi haujakamilika na hivyo kurudishwa mahabusu. 

Aidha mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Seth waliiomba mahakama imruhusu mteja wao akatibiwe nje ya nchi kwa madai kuwa ana uvimbe tumboni ambao umekuwa ukimsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi kwa takriban wiki ya nne. 

Hata hivyo ombi hilo limekataliwa mahakama na kuagiza kuwa mtuhumiwa huyo atibiwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili.


 ================ ==================











About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search