Gumzo: Mbowe vs DC Hai.. Mahakama yataka Mbowe aendelee na #Kilimanjaro Veggies yake.. #share

Mahakama kuu masijala ya Moshi (High Court Moshi Registry), imeruhusu shughuli za kilimo kuendelea kwenye shamba la kampuni ya Kilimanjaro Veggies inayomilikiwa na Mhe.Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, huku kesi ya msingi ikisubiriwa kusikilizwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Bw.Gelasius Byakanwa.



Katika kesi hiyo ambayo Kilimanjaro Veggies inadai fidia ya Millioni 549 kufuatia shamba lake kuingiliwa na kuharibiwa miundombinu yake na mshitakiwa huyo.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Aishieri Sumari wa Mahakama Kuu, ambaye ameeleza kuwa Mkuu huyo wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama walivunja sheria kwa kuvamia shamba hilo kwa kigezo kuwa lipo ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji. Mahakama imeelezwa kuwa shamba hilo lipo zaidi ya kilomita 20 kutoka chanzo cha maji (source of river Kikavu) na si mita 60 kama ilivyoelezwa na Mkuu huyo wa wilaya.
Imebainika kuwa mkuu huyo wa wilaya alihesabu mita 60 kutoka mtoni na si mita 60 kutoka chanzo cha mto kama sheria inavyoeleza. Sheria ya Mazingira Namba 20 ya mwaka 2004 inalipatia Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira (NEMC) mamlaka ya kuzuia shughuli za kibinadamu katika eneo la mita 60 kutoka chanzo cha maji/mto na sio mita 60 kutoka mtoni.

Kufuatia maelezo hayo ya Mahakama, sasa mkuu huyo wa wilaya atakabiliwa na mashtaka ya kuvunja sheria na kuvamia shamba hilo kisha kufanya uharibifu (akipatikana na hatia atalipa Shilingi milioni 549). Pia anashtakiwa kwa kuingilia kazi za Baraza la Taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC). Kwa mujibu wa sheria Nemc Ndio wenye mamlaka ya kuzuia shughuli kuendelea si mkuu wa wilaya. Na ikiwa Nemc watahitaji ulinzi watamjulisha mkuu wa wilaya/mkoa kwa maandishi, lakini Nemc wamekanusha kuomba ulinzi wowote kwa DC huyo.



DC Hai wakati wa 'Opereshen Maalum' katika shamba linalosemekana Mhe. Mbowe..
Aidha mshtakiwa huyo ameonywa kuacha tabia yake ya kukwepa kufika mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili bila sababu za msingi. Ameelezwa kuwa akiendelea kukaidi wito huo, mahakama itasikiliza na kufanya maamuzi upande mmoja (default judgment).
Kampuni ya #Kilimanjaro Veggies inawakilishwa na Wakili Menraid D'souza. Uamuzi huo umetolewa jana tarehe 13, July 2017, na Mahakama kuu, Masijala ya Moshi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search