Morning Talk: Shaka-shaka yatawala ajira 10,000 za Waziri Kairuki.. Uganda 'kuipa shavu' Bandari ya Dar es Salaam.. #share.. Khalfani Kikwete yu mgonjwa Hospitali ya Muhimbili..na Diamond Karanga 'yafunika mitaa' jijini Dar es Salaam..

SERIKALI ya Uganda imeamua kutumia usafiri wa maji kusafirisha bidhaa na huduma zake kutokana na unafuu kuliko njia ya reli inayoonekana kuwa aghali zaidi. Katika uamuzi huo, Uganda imechagua bandari ya Dar es Salaam kuwa sehemu yake ya kusafirishia bidhaa na huduma kwa kuwa ni nafuu na salama zaidi kuliko bandari zingine. 




Hatua hiyo inakuja wakati nchi hizo mbili zikitarajiwa kunufaika na bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga ambapo ushirikiano huo umeendelea kuleta manufaa kwa mawaziri wa sekta ya usafirishaji kuendelea na mazungumzo ya kuendeleza ukanda wa kati wa usafirishaji na uchumi endelevu. 

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati kusaini makubaliano katika usafirishaji kati ya nchi hizo mbili, Waziri wa Usafirishaji wa Uganda Henry Bagiire alisema Serikali yake inatamani kuboresha ukanda wa kati kama mkakati wa kuhakikisha wanafikia uchumi wa kati. 
Alitaja maeneo ambayo yanahitaji utekelezaji kuwa ni pamoja na kuboresha kivuko cha mv Kaawa, kuandaa bandari za Bell na Jinja na kuifanyia matengenezo bandari ya Bukasa. “Usafiri wa maji ndio chanzo kikuu cha kusafirisha bidhaa kirahisi, hivyo uchumi wa nchi yetu hautafanikiwa bila njia hiyo, hata ukingalia nchini ukitaka kusafirisha chai kwa reli unatumia dola milioni 120 kwa tani tena kwa ufanisi lakini kwa maji ni dola milioni 60,” alisema. 
Alisema ukitumika usafiri wa maji kwa kiasi kikubwa utaokoa dola milioni 40 kwa mwaka na kwamba kwa mwaka 2003 ukanda huo ulihudumia tani 330,000 sawa na asilimia 30. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema kufanikiwa kwa njia hiyo ya Uganda kusafirisha bidhaa zake kupitia bandari ya nchini kutaleta ufanisi kwenye sekta hiyo. “Uganda ni rafiki zetu, hivyo tunashirikiana nao kuhakikisha wanatumia bandari hii kwa kuwa itasafirisha mizigo kwa ufanisi kutoka Dar es Salaam-Mwanza hadi Kampala, kwa saa 24 tu,”alisema. 

Alisema suala hilo likisimamiwa vizuri, mizigo ya nchi hiyo itafikishwa kirahisi na kwa muda mfupi na kuondoa urasimu wa wateja kupewa risiti nyingi na badala yake watapewa moja tu ya gharama zote. 
Aliongeza kuwa pia utaleta faida kwa pande zote mbili, kwa kuwa ni wajibu kwa nchi hizo kutumia bandari za pande zote kwa kuwa ni ndugu kwenye masuala ya biashara. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko alisema kufanikiwa kwa makubaliano hayo, kutawezesha mizigo ya Uganda kusafirishwa kwa siku siku nne badala ya tano kupitia njia ya Mutukula.
============= =====end ===============

Chama cha Waajiri Tanzania (Ate) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), vimeipongeza Serikali kwa kutoa kibali cha kuajiri watu 10,184, lakini vimetaka kuwapo kwa umakini wakati wa kuajiri ili matatizo yaliyojitokeza awali yasijirudie.

Tahadhari hiyo imetolewa baada ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuruhusu taasisi na mamlaka zake kuajiri wafanyakazi wapya kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti.
Waliopewa vibali vya kuajiri ni mamlaka za Serikali za Mitaa, sekretarieti za Serikali za mikoa, wakala wa Serikali, taasisi na mashirika ya umma ambao baada ya uhakiki, walikabiliwa na upungufu wa wafanyakazi.

Watumishi wa umma watakaoajiriwa wanatakiwa kuripoti kazini kuanzia Agosti.
Akizungumzia uamuzi huo jana, mkurugenzi mtendaji wa Ate, Dk Aggrey Mlimuka alisema ni jambo zuri kwamba Serikali imetoa kibali cha ajira lakini taasisi na idara zinatakiwa kuwa makini wakati wa kuajiri.
“Serikali imepoteza fedha kwa ajili ya uhakiki wa vyeti. Wanapoajiri tena wanatakiwa kuwa makini kuajiri watu wenye sifa. Hiki si kipindi cha kujaza nafasi bali kutoa ajira kulingana na sifa za kazi wanazoziomba,” alisema.
Dk Mlimuka alisema nafasi hizo za ajira ni fursa muhimu kwa vijana ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ajira.
Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya alisema: “Tunafahamu huu ni mwanzo tu, lakini Serikali itaendelea kutoa ajira zaidi ya hizo kama ambavyo imekuwa ikiahidi.”
Alisema pamoja na kutangaza ajira hizo, bado Serikali inatakiwa kutekeleza ahadi yake ya kutoa ajira 52,000.
Nyamhokya alisema shirikisho likiwa mdau wa wafanyakazi linapenda kusikia kila mara ajira zikiongezeka.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso), Stanslaus Kadugalize alisema ni fursa kwa wanafunzi waliopo mitaani ambao wanahangaika na tatizo la ajira.
“Sina takwimu sahihi za wahitimu waliopo mtaani kwa sasa lakini nafahamu wapo maelfu wanazunguka mchana kutwa wakiwa na vyeti wanatafuta ajira,” alisema.
Hata hivyo, alisema changamoto iliyopo ni kwa waajiri kutaka watu wenye uzoefu wa kazi wakati wanapotangaza nafasi za ajira.
“Hii ni changamoto lakini tumeshaipeleka Sekretarieti ya Ajira ili ipatiwe suluhisho. Tunaiomba Serikali iendelee kutoa vibali zaidi na zaidi vya ajira,” alisema.
Jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki aliwataka waajiri kufanya uhakiki wa kina wa vyeti vya elimu wakati wa kuajiri ili kuwe na watumishi wa umma wenye sifa zinazostahili.
Akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam Kairuki alisema uhakiki wa kina utasaidia kuepuka kujirudia kwa suala la kughushi vyeti... 




============= ==============end=















About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search