GUMZO: Mbunge Kunti Majala wa CHADEMA ashikiliwa Polisi.. Raila ataka Wakenya wasikutane 'kimwili' siku ya Mkesha wa Uchaguzi.. #share.. Buriani Bi Linah George Mwakyembe...

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Kunti Majala alishikiliwa na polisi kwa zaidi ya saa tatu akidaiwa kufanya kusanyiko lisilo halali katika kijiji cha Mapango, kata ya Chandama wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana jioni.



Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Julai 18, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema mbunge huyo aliitwa na polisi kuhojiwa baada ya kupokea malalamiko kuwa alikuwa akiitukana Serikali na kutumia lugha chafu katika shughuli zake za kisiasa kwenye jimbo hilo.
Pia amesema mbunge huyo alikuwa akifanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali cha polisi.

Hata hivyo, Kunti amesema kuwa aliruhusiwa kufanya mkutano huo na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Chemba kwa njia ya simu.
Hata hivyo jana alipomaliza kuhojiwa, polisi walitoa barua ya kukataza mikutano yake ya hadhara aliyokuwa aifanye jimboni humo kuanzia jana hadi Julai 20 - mwananchi online..

========================================
Mgombea Urais nchini Kenya kwa tiketi ya Umoja wa Upinzani (NASA), Raila Odinga amewataka wananchi nchini humo kutokutana kimwili na wenza wao siku ya mkesha wa Uchaguzi Mkuu Agosti, 7. 



Odinga ameyasema hayo wakati akihutubia katika eneo la Homa Bay ambapo alisema wananchi wanatakiwa kujiandaa kwa uchaguzi ambao utafanyika Agosti, 8 na hivyo ni vyema siku hiyo wasikutane na wenza wao ili wajiandae kwa uchaguzi. 

Katika kusisitiza hilo amewataka hata ambao wapo kwenye ndoa kufata ushauri wake na akiwataka wanawake kuwanyima waume zao unyumba hata kama wakitaka kufanya nao mapenzi. 

“Tunakwenda kwenye vita tunahitaji kuwa na nguvu ya kutosha kabla hatujaingia kwenye vita Agosti 8, hakuna mtu kati yetu anatakiwa kufanya mapenzi usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi, “Wanawake wote wanapaswa kuwanyima unyumba haki yao kwa usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi,” alisema Odinga wakati akiwahutubia wananchi na kuongeza. 

“Tukifanya hivyo tutaweza kuamka mapema, tutapiga kura na kubakiwa tukiwa vizuri mpaka siku matokeo yanatangazwa.” alimaliza Bw. Odinga. Mo blog

==========================












About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search