INAUMA SANA..!! Baada ya lile povu la 'kumdetisha Ali Kiba' Queen Darleen sasa kaibuka na siri nzitoo.. #share
Baada ya 'mlipuko mtandaoni' uliozusha fununu za mahusiano kati ya Mkongwe wa Rymes katika anga za Bongo Ali King Kiba na Mrembo nyota mwenye uzuri wake Queen Darleen,..
anayefanya vizuri akiwa chini ya Lebo ya ‘WCB’, 'amefunguka' na kumwaga mtama hadharani kuwa anaumizwa sana na hali ya kuishi bila mpenzi jambo ambalo limekuwa likimuumiza sana katika maisha yake ya sasa, maana yeye pia anahitaji kupenda na kupendwa kama walivyo watu wengine.
Akichonga na Showbiz Xtra, Queen Darleen, ambae ni dada wa Boss wa WCB Diamond Platnumz, alisema kuwa,.. tangu aachane na mzazi mwenziye aliyezaa naye mtoto mmoja wa kike, hajawahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi jambo ambalo amekuwa akijiuliza bila kupata jibu kuwa linasababishwa na nini...?
“Naumizwa na hii hali,.. kuna wakati huwa nafikiria wanaume wananiogopa au sijui ni kitu gani kinatokea.. sasa nahitaji kuwa na mpenzi,” alisema Darleen - Crdts Bong Movie
No comments:
Post a Comment