Safari ya Muafaka ndani ya Chama; CUF Waanza kunyooshana !!

Katika kinachoonekana kama ni kuwarudisha kindini baada ya kutambuliwa rasmi na RITA, chama cha Wananchi CUF hususan kambi inayoongozwa na Process Lipumba.. imepania kuwaita Wabunge na Madiwani walio upande wa kambi ya Maalim katika kamati maalum ya nidhamu.
Matukio360 tumefaikiwa kupata kile  kilichotajwa kuwa ni waraka wa wito kwa viongozi hao ikiwataja baadhi yao kwa majina... na tunaendelea kufuatilia uhalisia wa waraka wenyewe kutoka ngazi husika..


===============
TAARIFA KWA UMMA
Imetolewa leo Jumamosi  Tarehe 22/07/2017
Cuf-Chama Wananchi
Kimewaita Wabunge wake 10 na Madiwani wake 2 Viti Maalum wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kutokana na sintofahamu iliopo ndani ya Cuf. Kamati ya Nidhamu na Maadili imekusudia kuwaita wale wote waliohusika kwa namna moja au nyengine katika mgogoro unaondelea ndani ya Chama. Watuhumiwa hao wataitwa kwa Makundi kama ifuatavyo
1. Kundi la Wabunge na Madiwani Viti Maalum
2 . Kundi la Wabunge na Madiwani wa Majimbo na Kata
3 . Viongozi wa Chama ngazi ya Wilaya
Kesho Jumapili Tarehe 23/07/2017 wafuatao wanahitajika mbele ya Kikao cha Kamati ya Nidhamu na Madili kitachofanyika Ofisi Kuu za Cuf Buguruni ukumbi wa Shaban Khamis Mloo saa  3:00 asubuhi .
1. Riziki Shahali Ngwali
2 .Saverina Mwijage
3 .Salma Mwassa
4 .Saumu Sakala
5 .Riziki Lulida
6 .Mgeni Jadi Kadika
7 .Raisa Abdallah Mussa
8 .Miza Bakari
9 .Halima Ali Mohammed
10 Khadija Al Kassim
11 Leila Hussein Madibi Diwani Viti Maalum Ubungo
12 Elizabeth Magwaja Diwani Viti Maalum Temeke
Wanachama hao watahojiwa mbele ya Kamati ya Maadili na kisha kufikishwa mbele ya Kikao cha Baraza Kuu siku hiyo hiyo saa  8:00 Mchana katika ukumbi huo huo wa Shaban Khamis Mloo.
Baada ya kukamilika kwa Mahojiano ya kundi la kwanza,  itafuatiwa  na makundi mengine katika muda utaopangwa
Mpaka sasa waliotajwa hapo juu, wamwshajulishwa kuhusu Kikao hicho, kwa hivyo Kikao kitafanyika kama kilivyopangwa.
HAKI SAWA KWA WOTE
Masoud Omari Mhina

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search