Good news!! James Foundation nao waja na kampeni 'zuia mimba' Mashuleni.... #share
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya James Foundation, Leonard Manyama amesema mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu taasisi hiyo itaanza kufanya Kongamano la Kampeni ya Maadili na malezi yenye lengo la kuwapa elimu wazazi na walezi ili kuwasaidia kuwaepusha mabinti walioko shuleni kupata ujauzito.
Akizungumza na Mwandishi wetu leo, mkurugenzi huyo amesema kongamano hilo litaanzia mkoani Dar es Salaam wilayani Kinondoni huku akisisitiza limebeba kauli mbiu inayosema Jifunze kusema hapana timiza wajibu wako.
''Wazazi watafundishwa malezi ya kuwalea vijana katika kila mkoa kongamano litafanyika katika kata na wilaya likishirikisha wadau mbalimbali,'' alisema Manyama.
Amesema elimu watakayopatiwa wazazi na walezi kwa kiasi kikubwa itawasaidia mabinti wanaosoma katika shule za sekondari kuwa na misimamo pamoja na kujitambua wakiwa shuleni wanatakiwa kuzingatia masomo na si vinginevyo.
Amesisitiza kuwa takwimu za Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi nchini (TACAIDS) zinaonyesha watoto wa kike wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19 ndio wanaongoza kupata ujauzito na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi huku akibainisha wengi wao wanaosoma shule hizo.
Ameongeza kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo wazazi na jamii nzima inatakiwa kutimiza wajibu utakaosaidia watoto wa kike kuwaepuka watu wanaowalaghai kusababisha kupata ujauzito unaopelekea kuwakatisha masomo yao.
Manyanya amesema mabinti hupata ujauzito wakiwa masomoni kutokana na sababu zikiwemo za wazazi kushindwa kutenga muda wa kuzungumza nao juu ya mabadiliko ya maumbile, elimu ya kujikinga na vishawishi, kutowatimizia mahitaji yao muhimu, kutowafuatilia mwenendo wa masomo yao na kujenga urafiki.
Amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwaficha watenda maovu hayo badala yake watoe ushirikiano kwa Serikali kufanikisha kuwatia nguvuni wale wote wenye wanaojihusisha na vitendo vya ngono na wanafunzi.
Amefafanua kuwa kampeni hiyo itashirikisha viongozi wa kisiasa, asasi za kiraia zinazopinga vitendo hivyo,walimu, Wanasaikolojia na kubainisha kuwa mashirika ya umma na binafsi yajitokeze kusaidia kufanikisha kongamano lifanyike kwenye mikoa mingine.
Aidha, amewaonya walimu wenye tabia ya kufanya ngono na wanafunzi kuacha kwani wao ndio wazazi na walezi wanapokuwan shuleni.
Na. Hussein Ndubikile

No comments:
Post a Comment