Sports news; Cheko, Nderemo na vifijo.. Kamati ya TFF ikimuachia huru Haji Manara #share
Kamati ya Nidhamu ya TFF imemfutia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa mwaka mmoja Afisa Habari Simba, Haji Manara.
Taarifa ya kina iliyapatikana kutoka vyanzo vya kuaminika zinasema, Haji hivi sasa yuko huria kuendelea na majukumu yake kama msemaji 'vuvuzela' wa simba..
Itakumbukwa mara baada ya kufungiwa, haji aliijia juu kamati ya nidhamu ya TFF kwa maamuzi aliyoyaita ya kionevu na kuapa kutetea haki yake kwa 'jasho na meno..'
Kupitia ukurasa wake wa instagram, manara pia alibainisha kwamba wakati wa maamuzi ya TFF alikuwa Zanzibar kikazi na akashangazwa na uharaka uliojitokeza.. na maamuzi bila ya yeye mlalamikiwa kusikilizwa..
Matukio360 tunaendelea kuwajuza yanayojiri klabuni Mzimbazi na kwa mtani Jerry Muro mara baada ya kuvuja kwa 'tetesi' hizi..
BAADA YA KUACHIWA MTANI HEBU MSIKIE MSANII NCHAMA THE BEST ANAYETAMBA NA KIBAO CHA “TUFANYE KESHO”: https://t.co/8ozfnx3h0x via @YouTube— AzamTV (@azamtvtz) July 17, 2017
No comments:
Post a Comment