Taarifa kutoka Jeshi la Polisi.. Kampeni zuia uhalifu sasa yawafuata 'wauza skerepa'.. #share

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imetangaza kuanzia jana kuanza operesheni maalum ya kupita katika maduka ya vifaa chakavu ili kubaini wahalifu wanaojishughulisha na wizi wa vifaa vya magari jijini.

Hayo yalibainishwa leo Jijini  Dar es Salaam na Kaimu Kamanda wa Polisi kanda hiyo DCP Lukas Mkondya akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuna watu ambao wamekuwa wakiiba vifaa vya kwenye magari na kwenda kuviuza tena.





“Tumeanza operesheni kali kabisa, sehemu zote kwa wale ambao wanaiba vifaa vya magari, mtu akipaki gari yake wanachukua powerwindow, wanachukua taa kuanzia leo (jana) nimewaagiza makamanda wote wa mikoa mitano, kuhakikisha wanasambaratisha vijiwe vyote na kuwabaini waharifu,” alisema DCP Mkondya.

Aidha alisema kuwa katika kufanikisha hilo, alibainisha kwamba operesheni hiyo pia itapita katika maeneo yote ambayo wamepewa taarifa za kuwepo kwa watu wanaojihusisha na biashara ya kuuza vitu vya wizi.

DCP Mkondya alibainisha kuwa watawakamata wote wenye maduka watakaobainika kufanya biashara hiyo na kutokana kutokana na hali hiyo watapita duka moja hadi jingine linalofanya biashara ya vifaa chakavu.

Aliwataka wote wenye magari kuorodhesha kwenye mafaili yao vifaa vya magari walivyonavyo na kueleza walipovitoa ambapo alibainisha kwa watakaoshindwa kufanya hivyo watakamatwa na kujumuishwa katika kundi la watu wanaojihusisha na shughuli hiyo haramu.

Alisema operesheni hiyo itakuwa enedelevu na kuwataka wananchi kutoa taarifa za watu na maduka yanayofanya biashara hiyo ili iwe rahisi kuwakamata na kuitokomeza katika jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine jeshi hilo Julai 16 mwaka huu maeneo ya Pemba Mnazi Kigamboni lilifanikiwa kukamata silaha moja aina ya SHOTGUN ikiwa na risasi tano ndani ya magazine.

Alisema silaha hiyo yenye namba za usajili TZ CAR 3421 ilikutwa ikiwa imetelekezwa na watu wasiojulikana katika maeneo ya ufukwe wa bahari ya hindi wakati askari wakifanya doria.

Aidha alisema silaha hiyo imehifadhiwa katika kituo cha polisi Kigamboni huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini mmiliki wa silaha hiyo ikiwa ni pamoja na kujua sababu ya kutelekezwa kwake.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search