Mabawa aja na Kampeni ya 'Magufuli Baki..' Kitaifa.. #share

Mtangaza nia wa nafasi ya Ubunge wa Chama cha Mapindunzi (CCM), Jimbo la Segerema katika Uchaguzi mkuu uliopita Bw. Laurence Mabawa, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kupokea Kampeni ya "Magufuli Baki" yenye lengo la kumpongeza, Rais John Magufuli kwa kazi anayoifanya na kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya utendaji kazi wa utawala wa awamu ya tano(5).


Akiongea na waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Idara ya Habari Maelezo leo, Bw. Mabawa amelaani vikali kauli na matamko yanayotolewa na baadhi ya Wanasiasa Nchini juu ya nia njema ya kampeni hiyo yenye lengo la kumpongeza Rais na Serikali yake,.. akiongeza kuwa Watanzania wanatambua kazi kubwa inayofanywa  na Rais Magufuli  ya kutetea na kupigania rasilimali za Taifa na Maslahi ya wananchi masikini wa Taifa hili  zinazofanywa na serikali yake... 

"Mimi kama Mtanzania mzalendo nimeamua kuchukua jukumu la kuanzisha kampeni ya "Magufuli Baki" kwa lengo la kupata maoni juu ya wananchi kuhusu utendaji kazi wa Rais," alisema Mabawa.

Alisema kampeni ya Magufuli, itahusisha Mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia Wananchi na kufanya nao mikutano  yenye nia njema ya kumuuombea Rais abaki katika msimamo wake wa kutetea Taifa.

Ameeleza kuwa kampeni hiyo inatoa fursa kwa wananchi kutoa maoni ya utendaji kazi wa Serikali kwa ujumla  kupitia mikutano na mitandao ya kijamii maalum iliyoandaliwa na kampeni hiyo.

"Pia  nawaomba Wanasiasa kuacha kutoa maneno ya makali na ya kuudhi yenye kumpinga Rais kwa kile anachokifanya..."alisema Mabawa.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search