MORNING TALK: CHADEMA yaja na 'fagio' kwa Prof. Lipumba,.. 'waziri ngeleja' 'katema mzigo kupitia CRDB Bank; angalia slip hapo chini.. Mosul huru na 'changamoto' kibao.. #share.. Ligi kuu Bara yaiva.. Kocha Mayanga aja na Mabadiliko kuivaa Rwanda..

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza operesheni maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).
Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.


Akizungumza jan wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa.
Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na viongozi wa CUF ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo mgogoro ndani ya chama, bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa Lipumba ambaye wamemuita kama ni msaliti.
"Sisi kama Chadema tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.
Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa Mameya wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba - Mwananchi

===== ==============end ====
Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ametahadharisha kwamba kuna changamoto nyingi, licha ya ushindi katika mapambano ya kuurudisha mji wa Mosul kutoka katika himaya ya wapiganaji wa Kiislamu. 



Mapigano ya miezi tisa yameharibu mji wa Mosul huku maelfu wakiwa wameukimbia mji huo na wengine wakiachwa bila makazi. Akizungumza mjini humo, bwana Abadi amesema hivi sasa ni muhimu kurudisha hali ya utulivu.

===============  ===== end ============





























About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search