News: TRA yawafunda wafanyabiashara wa kigeni,.. #share

WAFANYABIASHARA raia wa kigeni wanaokuja nchini kufanya biashara wametakiwa kufuata sheria na taratibu za ufanyaji biashara na ulipaji kodi ili kuisaidia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya mapato yatakayosaidia kukuza uchumi wa nchi.


Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es salaam na Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa mamlaka hiyo ,Diana Masalla katika semina iliyoandaliwa na Serikali ya Wilaya ya Ilala kwa kusshirikiana na Jeshi la Uhamiaji yenye lengo la kuwapa elimu juu ya sheria za uhamiaji,ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara kutoka China.

Alisema miongoni mwa wafanyabiashara kutoka china wamekuwa wakikamatwa kutokana na kushindwa kuzingatia na kufuata taratibu zinazoongoza masuala ya ulipaji wa kodi huku akisisitiza semina hiyo itasaidia kuondoa tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.

"Wito wangu kila mfanyabiashara anakuja nchini Kabla hujaanza kufanya biashara anata ajue sheria za kodi zinasemaje maana akipenda kinyume atachukua iwe hatua kulingana na sheria za nchi zinavyoeleza,"alisema Diana.

Diana alisema semina hiyo imeshirikisha zaidi ya wafanyabiashara 100 kutoka nchi hiyo na kwamba itakuwa endelevu kila watakapojulishwa idadi ya wafanyabiashara wa kigeni waliongia nchini.
Hata hivyo alisisitiza kuwa wafanyabiashara hao kutoa risiti wakati wanapofanya mauzo na wateja kudai risiti wanaponunua bidhaa.
Aliongeza kuwa kupitia semina hiyo wafanyabiashara hao wamepewa mafunzo yatakayowasaidia kuelewa aina ya msamaha ya kodi inayotolewa na taratibu za ufunguzi wa biashara.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Sophia Mjema alisema wameamua kukutana na wafanyabiashara hao kwani wengi wao wanafanya shughuli zao katika eneo la Kariakoo hivyo ni moja ya miakakat ya serikali kuhakikisha inapata mapato.

Naye Kaimu Afisa Uhamiaji wilaya ya Ilala Charles Washima alisema wageni wengi hawajui kanuni na taratibu za ufanyaji biashara nchini hali inayosababisha kukwaruzana na vyombo vya dola.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search