Picha 3: JK awasili msibani kumfariji Waziri Mwakyembe.. #share

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni wa watu mashuhuri waliowasili mchana huu nyumbani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe kumfariji na kumpa pole kufuatia kifo cha Mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 15/07/2017.

Dkt. akiwasili nyumbani kwa Dkt. Mwakyembe.
Dkt. Kikwete aliwasili msibani hapo majira ya saa tano asubuhi na kupokelewa na wenyeji wake na kisha kukutana na Dkt. Mwakyembe.

Ratiba ya mazishi inaonyesha marehemu Bi Linah anatarajiwa kuzikwa siku ya J'tano tarehe 19/07/2017.

Rais Mstaafu akilakiwa na wenyeji wake alipowasili msibani hapo.

Dkt. Jakaya akisaini kitabu cha maombolezo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search