RECORD: TRA imekusanya Trillioni 14.4 ikivunja Rekodi ya Mwaka jana kwa 7.67%.. Imewashukuru wadau #share
Mamlaka ya Ukusanyaji Mapato Tanzania TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs. Trillioni 14.4 kwa mwaka 2016/17 ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.67 ikilinganishwa na makusanyo ya mwaka 2015/16.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa Kodi Bw. Richard Kayombo alipoongea na Waandishi wa Habari kuwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha TRA kutinimiza malengo yake.
Matukio360 tumekuwekea waraka maalum wenye ripoti kamili kutoka kwa Bw. Kayombo.
No comments:
Post a Comment