Press Release:TCRA yazishushia rungu kampuni za simu, yazipiga faini kwa kusajili laini bila vitambulisho…# share
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitoza faini
kampuni zote za simu nchini kwa kosa la kusajili laini bila vitambulisho na
kutofuata utaratibu.
Hayo yalibeinishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari, alisema hii si
mara ya kwanza kwa kampuni hizo kutozwa faini kwa kukiuka sheria.
Alitaja kampuni hizo na viwango vya faini, alisema Airtel sh.
biloni 1.08, Smart sh. bilioni 1.3, Vodacom sh. milioni 945, Zantel sh. milioni
105 na Halotel sh. bilioni 1.6.
“Kutokana na kwamba zimerudia kosa tumeziongezea faini tena,
Airtel imetozwa sh. milioni 542, Smart sh. milioni 37, Tigo sh. milioni 625,
Zantel sh. milioni 52 na Halotel sh. milioni 822,” amesema.
Pia, kampuni hizo zimetozwa Sh. milioni 500 kila moja kwa kosa
la kuathiri na kuhatarisha usalama wa umma na jamii ya Watanzania kwa kusajili
laini bila kufuata utaratibu.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment