Wahenga hawakukosea waliposema teke-linalokujia (Tek-nolojia) ina madhara yake.. usemi huu umedhihirika jana baada ya mfumo wa usafiri wa magari yanayotembea angani Jijini cologne nchini Ujerumani, kukwama kwa masaa na kuacha watumiaji waliobakia angani na taharuki waasijue la kufanya.
Hayo yalijiri baada ya gari moja la angani kugonga nguzo na kusimama juu usawa wa mto Rhine nchini humo, hali iliyodumu kwa masaa na kusababiasha huduma ya zimamoto kufanya uokoaji kwa njia ya dharura ili kuwafikia zaidi ya abiria 75 waliokuwa wamekwama, huku baadhi yao wakiripotiwa kuwa umbali wa hadi mita 40 angani.
Jumla ya magari 32 yaliyokuwa angani wakati wa mkwamo huo walilazimika kusima kwa muda kupisha uokoaji, ingawa hakujaripotiwa vifo wala majeruhi hkatika mkasa wa jana.
 |
Vikosi vya uokoaji wkijitahidi kunusuru hali za abiria.. |
 |
Wazimamoto wakiendelea kuokoa baadhi ya watoto waliokwama... |
No comments:
Post a Comment