Court neWs: Baada ya Harbinder Singh na Rugemalila, leo ni zamu ya marais wa Simba na TFF mahakamani Kisutu.. #share

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Rais wa Simba, Evans Aveva, leo Jumatatu wanatarajia kupanda tena mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi zao zinazoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dares Salaam.



Marais hao wanatuhumuiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha ambapo wote wapo mahabusu kutokana na kunyimwa dhamana.

Washtakiwa wengine ambao wapo sambamba na kina Malinzi ni pamoja na Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa Fedha TFF, Nsiande Isawafo Mwanga pamoja na Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Kesi ya Malinzi na Mwesigwa inasikilizwa chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wibroad Mashauri huku kesi ya kina Aveva na Kaburu ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search