UBUNIFU: Baada ya 'Roboti ya Kitanzania..' Huyu hapa Mtanzania mwengine katuletea Mashine ya kisasa ya 'kutotolesha' mkaa.. #share..

MKURUGENZI wa Ubunifu wa Mashine ya Uzalishaji Mkaa na Mitambo ya Kukaushia Tumbaku, Leornad Kushoka amesema ubunifu aliotumia kubuni mashine ya kutolea mkaa unaotokana na taka utaweza kupungunza tatizo la ukataji miti ya misitu kwa ajili ya uchomaji mkaa kwa matumizi ya jamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
Akizungumza Dar es Salaam jana alisema mashine zinazotumika kutoa mkaa unatokana na taka utasiadia kupungunza soko la watumiaji mkaa kwa uchomaji miti ya misitu ovyo.

Alisema zaidi ya hekari 80,000 za eneo hili ni misitu iliyopandwa na hekari Milioni 1.6 hulindwa kama vyanzo vya maji,hifadhi ya wanyamapori,ufugaji wa nyuki na saikolojia asili .

“Watu wengi hutumia miti vibaya katika ukataji kwaa jili ya kuchoma kupata mkaa hali ambayo husababisha majanga mengi ikiwemo uharibifu wa mazingira ya misitu na kupoteza vyanzo vya maji na mvua hivyo nishati ya uzalishaji wa mkaa unaotokana na taka utasaidia kulinda na kupunguza uharibifu wa misitu katika nchi yetu,”alisema Kushoka.


Alisema kwa kutumia mashine ya kutengenezea mkaa unaotokana na taka na mabaki ya nafaka hali ambayo itasaidia pia kuwapatia kipato na kuacha ukataji miti ovyo kwa ajili ya kuchoma mkaa kwa matumizi ya kupikia.

“Ubunifu wa mashine yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mkaa mbadala amabapo mashine hii inauwezo wa kuzalisha mkaa kg 160 kwa saa na kuzalisha gunia zisizopungua 20 hadi 30 kwa siku kwa kutumia taka na mabaki ya nafaka kama karanga,mimiea,”alisema Kushoka.

Alieleza kuwa pamoja na ubunifu huo wameshaanza kuhamasisha jamii kuzalisha mkaa mbadala ndani ya miji mikubwa kwa kuamini kwamba kujishotoleza kwa mkaa mbadala kutaweza kupelekea kuuwa soko la mkaa wa miti.

Amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kupata elimu inayotolewa na Kampuni ya Tools Manufacture Group jinsi ya kupata semina fupi ya kufundisha kutengeneza mashine hizo na utengenezaji wa mkaa mbadala unaotokana na taka.


Mkurugenzi wa Ubunifu wa Mashine ya Uzalishaji Mkaa na Mitambo ya Kukaushia Tumbaku, Leornad Kushoka akiwaonesha Waandishi wa Habari namna mashine hizo zinavyofanyakazi 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search