gOOD nEWS: VETA na Ujermani waingia makubaliano kutoa mafunzo ya ujuzi wa kilimo kusaidia vijana kupata ajira....#share
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeingia
makubaliano na Serikali ya Ujerumani katika kutoa mafunzo ya kilimo kwa
vijana ili kuwaongezea ujuzi
wakuwasaidia kupata ajira.
Utiaji saini makubaliano hayo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam baina Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa
Wizara wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Moshi Kabengwe na Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo Reiner Nolten wenye lengo la
kutoa mafunzo ya kuongeza uzalishaji ya kilimo nchini.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kabengwe alisema mafunzo
hayo yatasaidia kuongeza ujuzi kwa vijana katika masomo na kuwa vizuri katika
elimu ya ufundi ambayo itawawezesha kupata ajira kwa urahisi.
“Mradi huu unamanufaa sana kwa vijana, utawasaidia kuwapa
ujuzi na kuweza kupata ajira, lakini pia kuendeleza nchi kiuchumi,” alisema
Kabangwe.
Balozi wa Ujermani nchini Defflef Waechoter ambaye alikuwa
shuhuda wakati wakutiliana saini, alisema Ujermani imeendelea kiuchumi kwa
kuwekeza katika mafunzo hayo ya kilimo hali ambayo imekuwa ikiwaingizia fedha
nyingi.
Alisema kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Ujermani wataendelea
kushitikiana na Serikali pamoja na Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya VETA Leah Lukindo Mfumo wa Wanagenzi
umeiletea maendeleo nchi ya Ujermani hivyo kwa kushirikiana nao wataweza kuleta
mapinduzi ya maendeleo nchini hususani katika sekta ya kilimo.
Aidha alisema wamekuwa wakiendesha mafunzo kwa vijana huku
wakishirikiana na waajiri, kutokana na hali hiyo wanafunzi wanapomaliza mafunzo
wanakuwa wameshajua hali ya mazingira kazi hivyo kuwa rahisi kuajiliwa.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment