bREAKING nEWS: Rais Kagame atwaa 98% ya kura, atangazwa mshindi kwa kipindi cha tatu.. #share

Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.



Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba.

Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa, Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana.

Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search