Breaking News: RC Makonda aendelea kukaangwa.. Tume nayo imemtupia zigo zito!! #share
Tume ya Kitaalamu iliyoundwa na Baraza la habari Tanzania (MCT) kwa ajili ya kuchunguza tukio la March 17, la uvamizi wa kituo binafsi cha Cloudz Entertainment, hatimae imewasilisha Ripoti yake.
Tume hiyo iliyokuwa chini ya Wakili na Mwanasheria Msomi Juma Thomas, ilipewa jukumu la kuchunguza uwepo wa ukiukwaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari na Uhariri.
Wakili Thomas, akiwasilisha Ripoti yake leo katika hafla maalum ya uzinduzi wa Ripoti hiyo, amesema katika kutimiza weledi wao, walifanikiwa kuwahoji Wafanyakazi wa Clouds, Mkuu wa Polisi Kinondoni, na waandishi wa Habari wakongwe, hata hivyo TCRA na RC Makonda mwenyewe walikataa Mahojiano nao.
Ripoti imebaini kuwa siku ya tukio RC Makonda alifika Cloudz akiwa ameambatana na Askari watano (5) jambo lililotafsiriwa kutumia mamlaka yake kufanya uvamizi na kuleta taharuki kwa Wafanyakazi wa clouds.
Mwisho, Tume imemtaka RC Makonda.. kukiri na kuiomba radhi menejimenti ya Cloudz Media Group Limited, na Tasnia nzima ya Habari Nchini.

No comments:
Post a Comment