bREAKING sPORTS: Yametimia Simba sasa kumilikiwa na Bilionea Mo-Dewji.....#share
Klabu ya Simba imepitisha rasmi mabadiliko mapya ya
uendeshaji wa klabu hiyo kuelekea kwenye mfumo wa hisa ambao kila mwananchama
anaweza kuwekeza hisa katika klabu hiyo.
Hayo yameafikiwa leo katika mkutano mkuu wa wanachama wa
klabu hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mwalimu Nyerere.
Awali akihutubia katika mkutano huo Rais wa Simba Salum Abdalla
amesema lengo la klabu ya Simba ni kuwa na shule ya michezo (Academy) viwanja
vya michezo na usajili mkubwa.
"Kukaribisha wawekezeji si kuuza timu, kuna utaratibu
unawekwa wa uwekezaji lakini sio kuuza timu kama ambavyo wengi wanadhani,”
amesema
Klabu ya simba itakuawa na uwezo kuboresha muundo wa
kiutawala na kujiwezesha kitaalmu, itaweza, kulipa mishahara, kutengeneza
Academy na miundombinu mingi inayo hitajika katika klabu kubwa kama Simba"-
katibu wa kamati ya mabadiliko bwana Selemani.
Bilionea Mo amekuwa akihitaji kwa muda mrefu kuwekeza katika
klabu hiyo kwa kumiliki hisa asilimia 51 huku 41 wakimilki wanachama. Hivyo hatua
hiyo iliyofikiwa leo ni ishara kuwa sasa matamaniyo yake yanakwenda kutimia.
Na Mwandishi Wetu




No comments:
Post a Comment