Hamad Rashid 'ajitosa tena mgogoro wa CUF'.. asema Maalim Seif 'mvurugaji' awataka meza ya Mazungumzo.. #share
MWENYEKITI Chama
Cha Alliance For Democratic
Change (ADC) Hamad Rashid amewataka viongozi wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Maalim Saif kumaliza mgogoro kwa vikao
badala ya kusubiri kesi zilizoko mahakamani.
Kauli hiyo
ameitoa leo akizungumza na viongozi na wanachama wa ADC katika maazimisho ya miaka
mitano tangu kuanzishwa kwa chama hicho, amesema mahakama kazi yake ni kuhukumu
tu lakini mgogoro utamalizika kwa njia ya mazungumzo.
“Ushauri
wangu wamalize matatizo yao kwa vikao na mazungumzo, mahakama haiwezi kumaliza
mgogoro bali inatoa hukumu tu, wao wamekuwa kila wanapokaa vikao ni kufukuzana,”
alisema Rashid.
Aidha amemshutumu
Maalim kuwa ni chanzo cha mgogoro huo kwani amekuwa hataki kusamehe na kuyamaliza
hadi kufikia hatua ya kumuwekea chuki Profesa Lipumba kwamba hawezi hata kumpa
mkono.
Rashidi ameongeza
kwa kusema kuwa amekuwa mtu mbinafsi ambaye anatataka analoamuwa yeye liwe
pasipo kusikiliza ushauri wa wengine. Kutokana na hali hiyo Rashid amesema
hataki viongozi wa jinsi hiyo ndani ya chama chao.
Amesema kufanya
siasa kunahitaji mtu mwenye hekima na busara ambapo alibainisha kuwa mwanasiasa
mzuri ni yule mwenye mbinu na mikakati mizuri isiyo na vurugu.
Kwa upande
mwingine amewataaka CUF- Maalim kuacha kueneza propaganda kuwa yeye ni msaliti
na kwamba ADC ni CCM “B” huku akibainisha kuwa Maalim ndiye msaliti kwani
haiwezekani kufanya mazungumzo na CCM peke yake bila kuwepo mashahidi wakujua
kinachozungumzwa kisha kukaa kimya.
Na Abraham Ntambara



No comments:
Post a Comment