bURUDANI: Staa Walper aanika mahusiano yake mapya.. asema watu hawafamu mazito anayokutana nayo kwenye mahusiano yake.. #share




Muigizaji wa filamu za Bongo Jacqueline Wolper ako na tabia ya kubadili wapenzi kila kukicha. Na sasa amekiri kuwa hatawacha tabia yake hio.

Wolper alipokuwa na mahusiano na Harmonize watu wengi walidhani mapenzi yao yatadumu lakini wawili hao waliachana na kila mmoja kupata mpenzi mpya.

Wolper akiwa na mahusiano na Harmonize
Wolper alijinyakulia kichana mwingine mchanga anayejulikana kwa jina la Brown ilhali Harmonize alipata mpenzi mpya mrembo wa kizungu.

Katika mahojiano na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wolper alikiri kuwa ataendelea kubadili wapenzi muda wowote atakapogundua kuwa aliyenaye hana vigezo.
Wolper na mpenzi wake mpya Brown
Mrembo huyo alieleza kuwa hawezi kuogopa maneno ambayo watu wanasema kwani hawaelewi anachokumbana nacho katika mapenzi, alisema kuwa hawezi kung’ang’ania kukaa kwenye uhusiano ambao haendani nao au unampa shida.

“Unajua unapokuwa na mpenzi huwezi kujua kuna tabia utakumbana nazo ambazo haziendani na wewe, lakini pindi unapogundua ni bora kuondoka kuliko kukaa sehemu ambayo huna furaha nayo,” alisema Jacqueline Wolper - Ghafla..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search