eLECTION nEWS: Mfahamu Diane Rwigara,.. mgombea wa kike wa Urais Rwanda 'anaemtikisa' Rais Kagame Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo 04/08/2017
Leo Agosti 4, 2017 wananchi wa Rwanda wanapiga kura
kumchagua Rais wa nchi hiyo. Wataamua kumchagua
aidha Rais aliyepo madarakani Paul Kagame, au
wapinzani wake Frank Habineza na Philippe Mpayima.
Wachambuzi wa siasa wanataraji kuwa Kagame ataibuka
na ushindi mkubwa katika uchaguzi huo. Hata hivyo, kuna
'sintofahamu' inayotokana na Katiba ya nchi hiyo
kubadilishwa mwaka juzi ili kumwezesha kiongozi huyo
kugombea muhula wa tatu, baada ya mihula miwili ya
miaka mitano kila mmoja.
Uchaguzi huo unaangalia kwa karibu na wafuatiliaji wenye
hofu kuhusu mmomonyoko wa demokrasia nchini humo.
Japo hofu hiyo inaweza kuwa ya msingi, lakini ni muhimu
iendane na ukweli kuhusu historia na maendeleo ya
kiuchumi ya nchi hiyo.
Rwanda inaweza kuelezwa kama demokrasia isiyo ya
kiliberali - 'demokrasia kipande,' 'demokrasia yenye
ombwe,' mfumo wa utawala ambao japo unaruhusu
chaguzi kufanyika, wananchi wananyimwa uelewa kuhusu
walioshika hatamu za utawala, kwa kunyimwa haki za
kiraia.
Hata hivyo, demokrasia hiyo isiyo ya kiliberali haipaswi
kugubika mafanikio makubwa chini ya utawala wa
Kagame, ambapo mwaka hadi mwaka, Rwanda imekuwa
ikipiga hatua kubwa kiuchumi. Kwa sifa hiyo tu, inatosha
kabisa kumfanya Kagame aibuke mshindi kwenye
uchaguzi.
Sasa tuwaangalie kwa kifupi wagombea urais katika
uchaguzi huo:
Kagame ni mgombea kwa tiketi ya chama tawala,
Rwandan Patriotic Front (PRF). Aliongoza waasi
waliofanikiwa kukomesha mauaji ya kimbari dhidi ya
Watutsi mwaka 1994. Kisha akawa Makamu wa Rais, na
mwaka 2000 akawa Rais katika serikali ya mpito.
Alichaguliwa kuwa Rais mwaka 2003, na akachaguliwa
tena mwaka 2010. Japo anaonekana kuwa maarufu, kuna
mgawanyiko mkubwa wa kimtazamo dhidi ya Kagame.
Kuna wanaomwona Kagame kama kiongozi wa kuigwa na
utawala wake mfano wa kupigiwa mstari, kwa kuzingatia
mafanikio makubwa katika ukuaji wa uchumi wanchi hiyo,
jitihada thabiti za kupunguza umasikini, mafanikio katika
sekta ya afya, kudhibiti rushwa, na kudumisha amani.
Mwaka juzi, Wanyarwanda walipiga kura kwa wingi
kuunga mkono Kagame aongoze nchi hiyo hadi mwaka
Lakini licha ya sifa hizo nzuri, kuna wanaomwona Kagame
kama mfano hai wa dikteta. Analaumiwa kwa kubana mno
fursa za kisiasa nchini Rwanda.
Mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu kama vile
Human Rights Watch na Amnesty International
yamemshutumu Kagame kwa kujenga mazingira ya kutia
hofu kwa mashambulizi dhidi ya wapinzani wake kisiasa,
wanatetezi wa haki za binadamu.
Frank Habineza ni kiongozi wa chama cha Deomcratic
Green Party of Rwanda kilichoanzishwa mwaka 2009
lakini kikazuiwa kusajiliwa hadi mwaka 2013. Mwaka
2010, Habineza alilazimika kukimbilia mafichoni kufuatia
kuuawa kwa Naibu wake, Andre Kagwa Rwisereka, lakini
akarejea nchini Rwanda mwaka 2012.
Habineza anatoa mbadala wa sera zilizoanzishwa na RPF,
ambazo anasema zimekuwa mzigo kwa Wanyarwanda.
Hizo ni pamoja na upanuzi mkubwa wa mazao na ardhi,
sambamba na umiliki wa ardhi na sera zinazoruhusu
utaifishaji wa ardhi kwa ajili ya matumizi ya umma.
Kwa upande wake, Philippe Mpayimana ni mgombea huru
asiye na rekodi yoyote ya kisiasa. Mwandishi wa habari
mstaafu, Philippe ameandika vitabu kadhaa kuhusu
mwenendo wa kisiasa na kijamii. Alikuwa akiishi
uhamishoni tangu 1994 hadi mapema mwaka huu.
Mpayimana anasema kwamba dhamira yake kuu ni
kuibadili Rwanda na kuwa nchi yenye demokrasia kamili.
Pamoja na mambo mengine, ameahidi kuimarisha taasisi
No comments:
Post a Comment