gOOD nEWS: Polisi yaua 13 Kibiti katika majibizano ya risasi....#share
WATU
13 wameuawa katika majibizano ya risasi baina yao na polisi katika eneo la
Tangibovu, kijiji cha Miwaleni Kibiti mkoani Pwani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika eneo la Tangibovu, kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti.
Taarifa
kutoka ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kuwa baada ya upekuzi, polisi walikamata
bunduki nane aina ya SMG pamoja na vifaa vingine.
Kuuawa
kwa watu hao ni mfululizo wa operesheni inayofanywa na Jeshi la polisi kuwasaka
watu waliokuwa wakifanya mauaji ya viongozi wa Serikali za vitongoji, askari wa
Jeshi la Polisi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambapo mpaka sasa
zaidi ya watu 37 wameshauawa kwa kupigwa risasi.
Jana
picha zilizotumwa na jeshi hilo katika vyombo vya habari zinamuonesha Mkuu wa
Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni
Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas
kuhusu mauaji hayo.
Katika
tukio hilo, mbali na silaha nane pia zilikamatwa risasi 158, pikipiki 2, pamoja na begi la nguo
vilivyokuwa vikitumiwa na
wahalifu hao.
Baada
ya kukagua vifaa vilivyokamatwa, IGP pia alizungumza na baadhi ya wananchi wa
Kibiti na kuwahakikishia usalama wa maisha na mali zao.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment