tREANDING nEWS: Bill Gates ateta na Rais Magufuli Ikulu, amtengea mabilioni ya fedha...#share

TAASISI ya Bill and Mellinda Gates imetenga takribani Sh. Bilioni 777.084  kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta ya kilimo, afya na mifumo ya kielektroniki ya upatikanaji wa taarifa hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ilisema Mwenyekiti Mwenza wa taasisi hiyo Bill Gates aliitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli .

Bill Gates amesema kama ambavyo taasisi yake imeshirikiana na Tanzania kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini, fedha hizo zitaelekezwa katika utekelezaji wa miradi zaidi ya afya ikiwemo kupunguza vifo vya uzazi, kukabiliana na ugonjwa wa malaria, kuimarisha lishe na kukabiliana na utapiamlo,

Aidha amesema zitaelekezwa katika sekta ya kilimo ambako zitasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao, kuzalisha mbegu bora na kuboresha ufugaji utakaoongeza chakula na pia zitasaidia kuweka mifumo ya kisasa ya upatikanaji wa taarifa.

Ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya uchumi wa Tanzania pamoja na uongozi na msimamo wa Rais Magufuli juu ya kutaka miradi hiyo ilete matokeo yenye manufaa, na kuahidi kuja hapa nchini mara nyingi ili kuimarisha zaidi ushirikiano na kufuatilia utekelezaji wa miradi.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Bill Gates kwa mchango mkubwa unaotolewa na taasisi yake katika miradi mbalimbali hapa nchini ikiwemo fedha ambazo taasisi hiyo itazitoa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa na kumhakikishia fedha hizo zinaleta matokeo yaliyokusudiwa.

Mazungumzo kati ya Rais Magufuli na Bill Gates yamehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Ufugaji na uvuvi Dk. Charles Tizeba na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search