bREAKING nEWS: Jeshi la Polisi lataja majina 13 ya watu waliouawa kwa tuhuma za ujambazi Kibiti...#share
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wanahabari
Tarehe 04.08.2017 huko eneo la Gari Bovu,
kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti, Wilaya ya Kibiti, Mkoa
wa Kipolisi Rufiji, Jeshi la Polisi lilimkamata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani akiwa ana majeraha maeneo
mbalimbali ya mwili wake akionekana kuwa alikuwa anaendelea kujitibia mwenyewe
kwa njia za kificho.
Mtuhumiwa huyu, alikamatwa
kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiintelijensia kuhusu yeye kuhusika na vitendo
vya kufadhili, kusaidia, kuhifadhi na kushiriki uhalifu wa ujambazi maeneo mbalimbali.
Mtuhumiwa alipohojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili alikubali na alionyesha
dhamira ya kwenda kuonyesha Ngome yao.
Ndugu Wanahabari
Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa
akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa
anashirikiana nao kufanya uhalifu.
Baada ya kukaribia
eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo
lililopelekea hata Abdallah Abdallah
Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake. Kufuatia
majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili.
Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali
majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati
tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu
nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao.
Miili ya marehemu
imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Jijini Dar es salaam.
Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa
7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza
maisha kutokana na majibizano ya risasi
wametambuliwa kuwa ni:
1.
Hassani
Ali Njame
2.
Abdallah
Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3.
Saidi
Abdallah Kilindo
4.
Abdulshakuru
Mohamed Ubuguyu
5.
Issa
Mohamed Mseketu @Mtawa
6.
Rajabu
Thomas @Roja
7.
Mohamed
Ally Kadude @Upolo
Miili
6 (sita) iliyobaki haikuweza
kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini
DSM.
Ndugu
Wanahabari
Vielelezo mbalimbali
vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
|
KIELELEZO
|
UTAMBUZI
|
SILAHA, RISASI NA MABOMU
|
||
1.
|
SMG = 5
|
Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
2.
|
Anti Riot Gun 38mm
= 2
|
Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
3.
|
SAR = 1
|
Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es
Salaam
|
4.
|
MAGAZINI = 2
|
Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
5.
|
Risasi za SMG 158
|
Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
6.
|
Bomu la kurusha kwa
mkono = 1
|
Uchunguzi dhidi ya
Bomu hilo unaendelea
|
7.
|
Mabomu ya kutuliza
ghasia = 4
|
Mali ya Jeshi la
Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
VIELELEZO VINGINE
|
||
8.
|
Pikipiki = 2
|
Pikipiki hizi
zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya
uhalifu maeneo mbalimbali
|
9.
|
Vitenge na Nguo
mbalimbali
|
Vitenge na nguo
mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi
|
10.
|
Begi = 1
|
Liliporwa baada ya
kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe
|
Ndugu Wanahabari
Kwa
mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na
utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu
maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili)
wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika
tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika
tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika
tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la
Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
Ndugu
Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi
ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:
a.Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya
kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa
Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba
wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia
mashaka.
b.
Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa
Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao
mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee
kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili.
c. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana
wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia
ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
d. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo
vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu
zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu
waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya
Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu
matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute
matibabu.
Kwa
hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa
maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na
walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.
Natoa
wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama
kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya
kufuata taratibu.
Ndugu
Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma
kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa,
Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao
bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi
la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa
Sheria mara moja.
Natoa wito kwa
wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo
chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Picha za watuhumiwa hao
zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.
Anafi
Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii.
Hassan
Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii.
Haji
Ulatule
iv.
Shekhe
Hassan Nasri Mzuzuri
v.
Rashid
Mtutula
Ndugu
Wanahabari
Nimalizie kwa kusema
kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri
sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi
kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu
nchini.
Imetolewa
na;
Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
No comments:
Post a Comment