nEWS: Mkemia Mkuu wa Serikali apiga marufuku wafanyabiashara kuingiza kemikali nchini....#share
OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepiga marufuku
wafanyabiashara wa kemikali kujishughulisha na uingizaji wa bidhaa hizo nchini bila kuwa na hati ya
usajili wa shughuli hiyo.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele ametangaza hatua
hiyo leo alipozungumza na waandishi wa habari,ambapo pia alipiga marufuku uingizaji
kemikali kabla ya kupata kibali.
“Uingizaji wa kemikali za viwanda na majumbani nchini kutoka
nje ya nchi unasimamiwa na chini ya Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali
(The Industrial and Consumer Chemicals (Management and Control) Act (ICCA), No.
3 of 2003),”alisema.
“Sheria hii katika sehemu ya tatu inamtaka kila anayeagiza
kemikali nchini ni lazima awe amesajiliwa kwa kuzingatia kifungu cha 11-28 na
awe amepewa hati ya usajili (Certificate of Registration) kama ilivyobainishwa
kwenye kifungu cha 29 kabla ya kuanza kujishughulisha na biashara,” alifafanua Manyele.
Amesema, sehemu ya pili ya sheria hiyo ya Mwaka 2015 kanuni
ya 3(1) (e) inaelekeza kila mdau wa kemikali aliyesajiliwa na kupata hati ya
usajili kuomba kibali ili kupata idhini kabla ya kuingiza mzingo wake nchini.
Manyere amesema wafanyabiashara wengi wamekuwa na utaratibu wa
kuagiza mzigo kwanza na inapowasili au kukaribia kuwasili ndipo wanaanza kuomba
kibali na wengine kuomba usajili kwa mara ya kwanza. Utaratibu ambao ni kinyume
cha Sheria ya ICCA.
Mkemia Mkuu huyo pia amepiga marufuku uingizwaji wa mizigo
yenye vifungashio vyenye maelezo ambayo hayako katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza
ambapo mzigo utakaokuja na maelezo yakiwa kwa lugha tofauti hautaruhusiwa
kuingizwa nchini.
Aidha ameeleza mzigo utakaoingizwa bila ya ‘label’
hautaruhusiwa kuingia bali utarudishwa ulikotoka kwani inaleta usumbufu katika
kuzihakiki.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment