GUMZO: Chid Benzi kanusurika 'Lupango',.. 'achekelea' miaka miwili ya kifungo cha nje.. atakiwa kuripoti polisi kila mwezi.. #share

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imewaweka chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka miwili Msanii wa Bongofleva Rashid Abdalah maarufu Chidbenzi na wenzake watano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo ya kuomba watuhumiwa hao wawekwe chini ya uangalizi kwa madai ya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.


Upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo hicho kwamba mahakama iwaweke chini ya uangalizi baada ya kubainikia kujihusha na matumizi ya dawa za kulevya.

Maombi hayo yalisikilizwa na jana jioni, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Ritha Tarimo.

Mbali na Chidbenzi, wengine watakaokuwa chini ya ungalizi ni, Hadia Abeid, Said Ally, Athuman Elias na Hassan Mohamed.

Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa upande wa Jamhuri unawasilisha hati ya kiapo  kutoka kituo cha polisi Msimbazi kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo mahakama itoe dhamana kwani wamekuwa na tabia mbaya katika jamii.

Glory alidai kuwa wanaiomba mahakama itoe amri ya kuwaweka wajibu maombi chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu na kusaidi dhamana ambayo itahakikisha wanakuwa na tabia njema na kutojihusisha vitendo vya dawa za kulevya.

Baaada ya kuwasilishwa kwa maombi hayo, Chidbenz na wenzake hakuwa na pingamizi.

Akitoa uamuzi hakimu alisema wajibu maombi watakuwa chini ya uangalizi wa polisi miaka miwili na kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaotia saini ya dhamana ya Sh.milioni mbili kila mmoja na kuripoti kituo cha polisi Msimbazi kwa mwezi mara moja.

hata hivyo, mjibu maombi Ally alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alirudishwa mahabusu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search