sPORTS nEWS: StarTimes kukuletea uhondo wa ligi kuu ya Bundesiliga kwa mara nyingine msimu wa 2017/18...#share
KAMPUNI ya StarTimes inatarajia kuonyesha matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu ya Ujermani (Bundesliga) msimu wa 2017/18 baada ya kupata haki ya kurusha ligi hiyo ambapo watazamaji wataweza kuona mechi zote kupitia king’amuzi cha startimes kuanzia Agosti 18.
Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Star Media Tanzania Zuhura Hanif wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuonyesha ligi hiyo, amesema kuwa wateje wake wote wataweza kuona mechi zaidi ya 300.
“Tunajivunia kuwaletea wachezeji maarufu, kama Robert Lewandowski, Franck Ribery na Thomas Mueller moja kwa moja, kwenye Luninga yako. Mpira huu utavutia mashabiki wengi na ukiangalia Bayern Munich ni moja ya timu kubwa itakayo kuwa ikicheza katika msimu huu,” amesema Hanif.
Aidha amesema katika msimu mpya wa mpira unaoanza, startimes itawaletea ligi kali kwa wateja wao ili waweze kufurahia maudhui bora wanayowapatia kwa kuangalia moja kwa moja kupitia chaneli zao za mpira ambazo zinapatikana kwenye king’amuzi hicho.
Hanif amesema lengo la kufanya hivyo ni kumwezesha kila shabiki wa mpira aweze kufurahia kwa gharama nafuu na kuaangalia ligi nzima huku wakifurahia kuangalia timu kubwa kama Bayern Munich, Bayern 04 Leverkusen na Burusssia Dortmund.
Amesema licha ya wateje wa StarTimes kufurahia ligi ya Bundesliga, wataweza pia kuangalia ligi kuu ya Italia (Serie A), ligi kuu ya Ufaransa (League 1), ligi kuu ya Uingereza (PL), ligi kuu ya Ubelgiji (Belgium pro league) na mwakani kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi.
Meneja Uendeshaji wa Star Media Gaspa Ngoi amesema kupitia mfumo mpya wa malipo ya king’amuzi mteja ataweza kulipa kuanzia Mambo sh. 12000 kwa mwezi, sh. 4000 kwa wiki n ash. 1000 kwa siku.
“Hii ni katika kuwahamasisha wateja wetu kulipia vifurushi tulivyonavyo ili kuweza kutazama chaneli na vipindi vingi zaidi tulivyonavyo vya kitaifa na kimataifa,” amesema Ngoi.

Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment