GUMZO: 'Onyo la mwisho' kwa Wakili 'msomi' Tundu Lissu afike Mahakamani kujitetea katika kesi yake ya 'dikteta uchwara'.. #share..

Mbunge kutoka mkoa wa Singida, Na Mwanasheria wa CHADEMA ambae pia ni Rais wa TLS, Wakili 'msomi' Tundu Lissu, bado yupo kwenye headlines za mambo ya kimahakama.

Siku ya jana ya August 08/2017 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ilimpa onyo la mwisho Tundu Lissu kuhakikisha anafika katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mahakamani hapo.




Onyo hilo lilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi kudai shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa Lissu hakufika Mahakamani kwa mara nyengine.

Wadhamini wa Lissu hawakufika pia Mahakamani huku Wakili wa Lissu Jeremiah Mtobesya akidai kuwa mteja wake alipata udhuru ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu alisema hiyo ni mara ya pili Lissu hajafika katika kesi hiyo hivyo anatoa onyo la mwisho ahakikishe anafika.

Hakimu huyo amesema kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa ambapo baada ya maneno hayo akaahirisha kesi hadi August 14/2017.

Katika kesi hiyo ya uchochezi (Dikteta uchwara) Lissu anadaiwa alitenda kosa hilo July 28/2016 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ilala Dar es Salaam

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search