GUMZO: Vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali 'vyamtia matatani' Billionaire Yusuf Manji... 'vyaonyesha anatumia dawa'.. #share

SHAHIDI wa Kwanza katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Yusuph Manji amedai mahakani kuwa uchunguzi Wa mkemia Mkuu umeonyesha Manji anatumia dawa za kulevya.

Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa jamuhuri, Ramadhani Kingai ambaye no Naibu Mkuu wa upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amedai hayo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akiongozwa na Wakili Wa Jamuhuri, Timon Vitalis, Kingai amedai, February 9 mwaka huu aliambiwa kufanya uchunguzi wa suala lililoripotiwa na Mkuu wa mkoa Wa Dar es Salaam Paul Makonda  juu ya watuhumiwa wa dawa za kulevya wakiwemo Josephat Gwajima na Yusuph Manji. 

Amesema alimuelekeza Dutektivu Koplo Sospter kuwapeleka Manji ambaye alifika katika kituo cha polisi mwenyewe na Gwajima kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kupimwa juu ya tuhuma hizo za dawa za kulevya ambapo baadae walipata taarifa kuwa Manji anatumia dawa za kulevya.
Alidai baada ya ripoti hiyo, alielekeza Manji afunguliwe jalada la kutumia dawa za kulevya kisha kwa DPP ambaye alimfungulia mashtaka

Hata hivyo shahidi Kingai alipoulizwa nani alielekeza kuwa dawa anazodaiwa kutumia Manji ni Heroine alidai, yeye alifanya upelelezi tu ila anayeandaa mashtaka in DPP.

Naye shahidi wa pili Koplo Sospeter amedai alipokea maelekezo juu ya mtuhumiwa Manji ambapo moja ya maelekezo hayo yalikuwa yakimtaka kumpeleka Manji  kwa mkemia Mkuu kwa ajili ya kupima sampuli  ya mkojo ambapo baada ya kufuata taratibu za ofisi ya mkemia na kupata namba ya maabara alimpeleka Manji msalani ambapo aliweka mkojo kwenye chupa maalumu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Amedai Februari 10, mwaka huu  majibu yalitoka na akakuta yanasema mkojo wake una chembechembe za dawa za kulevya.
Kesi hiyo itaendelea Leo..


 Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiteta jambo na Wakili wake, Hudson Ndusyepo wakati wakiwa ndani ya mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam leo kabla ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.


Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akisubiri  kusomewa kesi ya Madawa ya Kulevya inayomkabiri.
 Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiwa ndani ya ukumbi wa mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam akisubiri kusomewa mashtaka yanayo mkabiri.
Mazungumzo yakiendelea.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search