gUMZO: Yule 'kigogo wa CCM' aliyejifanya Afisa Usalama(TISS) Mkoani Arusha aongezewa shtaka la kughushi nyaraka.. hatimae kapanda kwa 'pilato' kujibu mashtaka yake... #share..

Siku ya jana ya 11/08/2017, Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .


Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho)

Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serekali Penina Joakim  amesema kuwa Mnamo May 18 katika hotel ya Skyway iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .

Wakili Penina alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .

Chanzo: Cloudsfm Redio

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search