Kauli ya Rais wa PSG ya Neymar No.1,.. yawakwaza Ronaldo, Messi.. #share
Wachezaji 'grade one' na nyota wa wakati wote(superstars of ALL-Time) Christiano Ronaldo na Leonel Messi wameonekana kumbeza vikali Rais Tajiri wa Club ya Paris Saint Germane (PSG) AL-KHALAIFI kwa kauli yake ya hivi karibuni ya Neymar No.1 iliyomshawishi kuvunja kibubu, na kutoa kitita cha pauni za Kingereza £ 222 million kumnasa nyota Neymar na hivyo kuvunja Mara-dufu record ya dunia ya uhamisho katika soka
Mtandao mmoja wa utani wa mambo ya kisoka umechapisha kibonzo cha wachezaji hao wakimtolea macho na kumkebehi Al-khalaifi, na kusema kwamba kumuweka Neymar no.1 kuwazidi wao katika 'radar za kisoka' hakuna mashiko, na kutaja sababu ya kumsifia kuwa ni kwa sababu Al-khalaifi amekosa 'fungu nene' la kuweza kuwanunua wao (Ronaldo na Messi).
No comments:
Post a Comment