Kutoka Mahakamani Kisutu:Bilionea Yusuf Manji hakufika mahakamani leo kisa...anaumwa!! #share
MFANYABIASHARA
na Mmiliki wa Makampuni ya Quality Group Yusuf Manji, ameshindwa kufika
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwenye kesi ya tuhuma za
Uhujumu uchumi inayomkabili kwa kuwa ni mgonjwa.
Taarifa hiyo
ilitolewa jana Wakili wa Serikali, Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Godfrey Mwambapa kwamba amepata taarifa kutoka kwa askari Magereza kuwa Manji
anaumwa na amepewa siku mbili za kupumzika.
Baada ya
Wilson kuieleza hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25
mwaka huu kwa kutajwa. Hata hivyo, Wilson alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
bado haujakamilika, akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Licha ya
Manji kutofika mahakamani kwa sababu za kiafya, washitakiwa wenzake Deogratius
Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere walifika mahakamani hapo kama
ilivyoelekezwa na Mahakama .
Awali,
Mahakama hiyo ilikataa kutoa kibali kwa upande wa mashitaka kumchukua Manji kwenda
kuhojiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), kuhusiana na masuala ya kodi.
Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha alisema hawezi kuruhusu ombi hilo kwa
sababu kesi iliyopo mbele yake ni ya uhujumu uchumi ambayo haihusiani na
masuala ya kodi.
Katika
mashitaka yanayomkabili Manji na wenzake Inadaiwa Juni 30, mwaka huuu maeneo ya
Chang’ombe A wilayani Temeke Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja,
walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo 35 ya vitambaa vinavyotumika
kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya Sh milioni 192.5.
Ilidaiwa kuwa
Julai Mosi mwaka huu, maeneo ya Chang’ombe A, wilayani Temeke, Dar es Salaam,
washitakiwa wote walikutwa na askari
polisi wakiwa na mabalo nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za
JWTZ vyenye thamani ya Sh milioni 44.
Katika
mashitaka ya tatu, inadaiwa Juni 30, mwaka huu maeneo ya Chang’ombe A, washitakiwa walikutwa wakiwa
na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa ‘’Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha JWTZ’’ bila kuwa na uhalali
kitendo kinachohatarisha usalama wan chi.
Pia inadaiwa,
terehe hiyohiyo maeneo ya Chang’ombe washitakiwa walikutwa na mhuri uliokuwa
umeandikwa ‘’Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupora Dodoma bila kuwa na uhalali
kitendo kinachohatarisha usalama.
Na Mwandishi Wetu




No comments:
Post a Comment