nEWS: Lema 'awatemea cheche' viongozi wa dini nchini....Adai wanajifanya hawaoni kinachoendelea...Awataka wachukue hatua....#share


Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amewataka viongozi wa dini nchini kuna kuwa wanawajibu wa kukemea vitendo vya udhalilishari wanavyofanyiwa wabunge wa upinzani.


Kauli hiyo ameitoa leo Mjini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akitoa rai kwa viongozi hao kutokemea tu matumizi ya viroba na bia.

Amesema kwa kusema kuwa viongozi wa dini mbalimbali nchini wasifumbe macho yao na kujifanya hawayaoni mateso wanayopata viongozi wa upinzani nchini.

"Viongozi wetu wa dini wasijifanye hili tunalofanyiwa upinzani hawayaoni. Kazi ya viongozi wa dini siyo kukemea bia na viroba bali wanatakiwa wapige kelele kwenye ukiukwaji wa misingi ya sheria inayoendelea hapa nchini dhidi ya upinzani", amesema Lema.

Aidha Lema ameongeza kuwa viongozi wa dini endapo watasimama katika kukemea maovu yanayofanywa ndani ya nchi yakiwepo ya unyanyasaji watakuwa wamelikomboa taifa kwenye machafuko.

"Ipo siku  kuna watu watashindwa kuvumiliwa haya tunayofanyiwa, hapo ndipo vita vya wenyewe kwa wenyewe vitakapokuja hapo siku za mbeleni" amesema.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search