sPOTRS : Jua wachezaji 8 wakuchungwa kuelekea mtanange wa Simba na Yanga ngao ya jamii kesho kutwa...#share
Wakati tukielekea kutizama mpambano wa ufunguzi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara (Ngao ya Jamii) katika ya Simba na Yanga, wafuatao ni wachezaji
wa kuchungwa na pande zote.
Simba na Yanga zitashuka dimbani siku ya Jumatano,
Agosti 23 uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kuwania Ngao ya
Jamii.
Ukiachana na historia ya pambano hilo, pia ukubwa wa mtanange
huo unatokana na nyota wapya waliopo kwenye klabu zote mbili.
Timu zote mbili zinatarajiwa kuwakosa nyota wake muhimu wa kikosi
cha kwanza kutokana na majeraha wanayouguza, Kakolanya, Mwashiuya na
Chirwa kwa upande wa Yanga wanatarajiwa kukosekana huku Bocco, Kapombe,
Mohammed Hussein kwa upande wa Simba wakiwa na asilimia kubwa ya kuukosa
mchezo huo.
Hawa ndiyo wachezaji 8 wa kuchungwa kuelekea mchezo
wa Yanga na Simba.
Amissi Tambwe - Yanga
Amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Simba tangu ajiunge na
Yanga misimu 3 nyuma, Mrundi huyo anaitaji ulinzi mkubwa kumzuia hasa kwa
mipira ya hewani, kama kona na krosi.
Shiza Kichuya - Simba
Ni mwiba kwa upande wa Yanga siku ya Jumatano, mechi
mbili za mwisho winga huyo aliibuka shujaa, safu ya ulinzi ya Yanga
inaitaji umakini mkubwa na kutoruhusu kufanya faulo maeneo ya karibu kwani,
Kichuya ni mpigaji wa mipra ya adhabu.
Donald Ngoma - Yanga
Ni mshambuliaji mwenye kasi, nguvu na jicho la goli, pia
ni mzuri kwenye mashambulizi ya kushutukiza, ana tazamiwa kuwa mwiba kwa
Simba kama asipowekewa ulinzi dhabiti wa kumzuia.
Emmanuel Okwi - Simba
Okwi ni mchezaji hatari sana kasi yake, krosi murua na
umakini wa kufunga amekuwa akiwapa tabu mabeki wengi hivyo safu ya ulinzi ya
Yanga inaitaji umakini wa kumdhibiti.
Thabani Kamusoko -- Yanga
Ndiye kiunganishi wa timu ya Yanga, kuanzia safu ya ulinzi
hadi ushambuliaji, hatakiwi kuwa huru kufanya anachotaka kwani ndiye mwenye
mipango yote ya klabu ya Yanga.
Haruna Niyonzima - Simba
Amejiunga na Simba akitokea Yanga, Harruna anatazamiwa kuwa
mwiba kwa upande wa Yanga kama asipowekewa ulinzi mkali, ni mchezaji mbunifu
mwenye uwezo wa kufunga, na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji.
Ibrahim Ajibu - Yanga
Siyo mshambuliaji wa kupewa nafasi muda wote, Ajibu ni mmoja
wa nyota wachache kwenye Ligi Kuu wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kutokana
na ubunifu wake mkubwa.
Mzamiru Yassin - Simba
Ni mchezaji ambaye atamkwi sana, ila ni mmoja wa nyota wa
kuangaliwa sana kwani mechi nyingi ngumu kwa upande wa Simba amekuwa ndiye
msaada mkubwa sana.
Na Jerry Mlosa/Goal Tanzania




No comments:
Post a Comment