sPORTS nEWS: Kauli ya Kiungo Mpya wa Simba Haruna Niyonzima kwa wenye maswali juu yake baada ya kutambulishwa mapema leo...#share
KIUNGO mpya wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima amesema hana
maneno mengi ya kuongea na kwamba majibu ya maswali mengi yanayoulizwa
yataonekana uwanjani kuanzia kesho.
Niyonzima amezungumza maneno hayo leo mbele ya Waandishi wa
Habari makao makuu ya klabu hiyo alipokuwa akitambulishwa pamoja na nyota
wengine Emmanuel Okwi na Nicholas Gyan.
Kiungo huyo ambaye ametokea Yanga baada ya kumaliza mkataba
wake mwezi uliopita amesema kwa sasa yeye ni mali halali ya Simba na mambo
mengine atajibu uwanjani.
“Mimi ni rasmi mchezaji halali wa klabu ya Simba, sina mengi
zaidi ya kuongea kikubwa tukutane uwanjani,” alisema Niyonzima.
Niyonzima, Okwi na Gyan wanatarajiwa kuongeza hamasa ya
mashabiki wa Wekundu hao katika mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya Rayon Sports
ya Rwanda katika Tamasha la Simba Day.
No comments:
Post a Comment