nEWS: Viongozi Chadema kuunguruma kesho jijini Dar es Salaam juu ya haya.....#share
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kesho
kutoa azimio jingine la Kamati kuu ya Chama iliyoketi Julai 29 hadi 30 mwaka
huujijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kuhusu mwenendo wa nchi.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari
wa Chadema Tumaini Makene, amesema uongozi wa juu wa chama hicho utazungumza na Umma kupitia vyombo vya habari.
“Uongozi wa juu wa chama kesho, utazungumza juu ya azimio
jingine la Kamati Kuu ya Chama iliyoketi Julai 29-30 jijini Dar es Salaam
kujadili masuala mbalimbali kuhusu mwenendo wa nchi kwa sasa,” amesem.
Ametaja moja ya azimio litakalozungumziwa ni azimio ambalo
lilihusu kuporomoka kwa uchumi wa nchi na hali ngumu ya maisha inayowakabili
Watanzania lilitolewa Julai 31, mwaka huu kwa umma kupitia mkutano wa
Wahariri/Waandishi waandamizi na uongozi wa juu wa chama hicho.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment