sPORTS nEWS: Simba kukipiga na Mtibwa Jumapili, kisha kumwendea Yanga mafichoni....#share
TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Soka ya Simba Jumapili hii ya tarehe 13-8-2017,saa kumi alasiri itashuka kwenye Uwanja mkuu wa Taifa hapa jijini kucheza na Klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo ni muhimu kwa pande zote mbili kujiandaa na Ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Simba pia tutautumia mchezo huo kuiwinda klabu ya Yanga, ambayo tutacheza nayo August 23 mwaka huu, kwenye mchezo wa kugombea Ngao ya hisani.
Baada ya mchezo dhidi ya Wakata miwa hao,Simba inatarajiwa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mawindo hayo
muhimu.
IMETOLEWA NA... HAJI S. MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
No comments:
Post a Comment