tREANDING nEWS: Kauli ya kwanza ya Rais Paul Kagame kuhusu Tanzania baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa mara ya tatu ...#share
RAIS wa Rwanda Paul Kagame ameahidi kuendeleza undugu na ushirikiano baina ya Rwanda na Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya wa nchi hizo.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kupokea pongezi kutoka kwa Rais John Magufuli kufuatia ushindi wake wa kiti cha urais kwa mara ya tatu.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa twitter kisha Rais Kagame kushukuru na kutoa ahadi hiyo.
Mawasiliano yao yalikuwa kama inavyoonekena hapa chini.
Rais Kagame ametangazwa jana kushinda kiti hicho kwa asilimia 98 katika uchaguzi uliofanyika juzi. Kagame amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba na kufuatia ushindi huo sasa atahudumu
muhula wa tatu wa miaka saba.
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa
kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari
ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa, Wapinzani wa bwana Kagame
walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana.
Rais Kagame aliingia madarakani
mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na
kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo
wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa
mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka
2034.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment